-
Katz amtusi vikali Erdogan baada ya mahakama ya Uturuki kutoa hati za kukamatwa viongozi 37 wa Israel
Nov 10, 2025 02:47Waziri wa vita wa utawala wa kizayuni wa Israel, Yisrael Katz amemshambulia kwa matusi makali Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan baada ya mahakama ya nchi hiyo kutoa hati za kukamatwa viongozi 37 wa utawala huo ghasibu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kimbari ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Slovenia: Tunaunga mkono kuanzishwa taifa la Palestina; mauaji ya kimbari yametokea Gaza
Nov 09, 2025 23:48Rais Nataša Pirc Musar wa Slovenia ametangaza kuwa, nchi yake inaunga mkono kuanzishwa kwa taifa la Palestina."
-
Kwa nini China inakosoa hatua za Marekani huko Yemen?
Nov 09, 2025 22:52Sun Lei, naibu mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amepinga madai ya mwenzake wa Marekani katika kikao cha Baraza la Usalama na kusisitiza kuwa: Washington imekiuka sheria za kimataifa kwa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Yemen na kusababisha mateso kwa raia.
-
Kususia Trump mkutano wa G20; sera za mashinikizo au mshikamano na Israel?
Nov 09, 2025 09:30Rais wa Marekani alitangaza kuwa, hakuna maafisa wa Marekani watakaohudhuria mkutano wa kila mwaka wa Kundi la G20 huko Johannesburg, Afrika Kusini.
-
Rais wa Colombia amshambulia Trump: Wewe na marafiki zako ni waongo
Nov 09, 2025 06:59Rais wa Colombia, Gustavo Petro, amemshambulia Rais wa Marekani, Donald Trump, akionya kwamba kinachoendelea huko Gaza kinaweza pia kutokea Kusini mwa Dunia.
-
Mamia watoweka baada ya boti kuzama katika mpaka wa Malaysia na Thailand
Nov 09, 2025 05:56Mamlaka ya Usafiri wa Baharini ya Malaysia imetangaza kwamba takriban watu 290 bado hawajulikani walipo leo Jumapili baada ya boti iliyokuwa imebeba watu wapatao 300 kuzama karibu na mpaka wa Malaysia na Thailand, huku manusura 10 wakiokolewa na mwili mmoja kupatikana.
-
Russia yaimarisha maandalizi ya vita ya nyuklia kufuatia maagizo ya Rais Putin
Nov 09, 2025 04:07Wizara ya mambo ya nje ya Russia imeanza kuchukua hatua za kutathmini uwezo wa taifa katika nyanja za nyuklia, kufuatia maagizo ya Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov.
-
Maandamano Paris kulaani mauaji ya halaiki Sudan, UAE yashutumiwa kwa kuunga mkono RSF
Nov 09, 2025 03:56Mamia ya waandamanaji walikusanyika Jumamosi karibu na Mnara maarufu wa Eiffel mjini Paris kulaani mauaji ya halaiki yanayoendelea nchini Sudan, huku wakiishutumu serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuwafadhili na kuwapatia silaha waasi wa RSF wanaotekeleza mauaji ya raia.
-
Palestina: Hati zilizotolewa na Uturuki za kukamatwa viongozi wa Israel ni 'ushindi kwa haki'
Nov 08, 2025 23:59Palestina imesifu na kupongeza hatua ya Uturuki ya kutoa hati za kukamatwa viongozi 37 wa utawala wa kizayuni wa Israel na kuielezea kuwa ni 'ushindi kwa haki' huku ikizitolea mwito nchi zingine kufuata mfano wa Ankara.
-
Zawadi ya dola trilioni moja kwa Musk mkabala wa njaa inayowakabili Wamarekani milioni 42; Uadilifu au mkanganyiko?
Nov 08, 2025 23:20Huku mamilioni ya Wamarekani wakihangaika kumudu milo yao ya kila siku, wanahisa wa Kampuni ya Tesla wamepasisha kifurushi cha fidia ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha dola trilioni moja kwa Elon Musk. Tofauti na kukinzana huku kukubwa kati ya utajiri wa mtu mmoja na umaskini uliokithiri wa mamilioni ya watu kumefichua taswira halisi ya pengo la pato nchini Marekani.