-
Dunia yalaani mashambulizi ya kigaidi ya Israel nchini Qatar
Sep 09, 2025 23:24Mashambulizi ya anga ya Israel huko Doha, Qatar, yaliyowalenga viongozi Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas, yameendelea kulaaniwa na nchi na viongozi mbali mbali kote duniani.
-
Kwa nini utawala wa Israel na Australia zinaendelea kushirikiana nyuma ya pazia licha ya mivutano ya kidiplomasia?
Sep 09, 2025 22:57Katika hali ambayo uhusiano wa kidiplomasia kati ya utawala wa Kizayuni na Australia umefika kiwango cha chini na kufutwa kwa viza za wanadiplomasia kumezidisha mivutano; lakini pande mbili hizo zinaendelea kushirikiana katika masuala ya kiusalama, kiteknolojia na kiuchumi.
-
BRICS inawezaje kuwa na nafasi muhimu na kuu katika kukabiliana na mwenendo unaotia wasiwasi wa hatua za upande mmoja?
Sep 09, 2025 08:46Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza katika mkutano wa dharura wa viongozi wa kundi la BRICS uliofanyika kwa njia ya video kwamba: BRICS inaweza kuwa na nafasi muhimu na kubwa katika kukabiliana na mwenendo unaotia wasiwasi wa hatua na misimamo ya upande mmoja.
-
Wasomi waliowasilisha lalamiko dhidi ya UK: 'Ghaza ni matokeo ya moja kwa moja ya Azimio la Balfour'
Sep 09, 2025 06:59Kundi moja la Wapalestina limewasilisha lalamiko la kisheria dhidi ya serikali ya Uingereza likidai kutolewa ungamo na fidia kwa jinai za kihistoria zilizofanywa na Uingereza huko Palestina kuanzia mwaka 1918 hadi 1948.
-
Kamanda Mkuu wa Ukraine akiri: Warussia wametushinda katika mstari wa mbele wa vita kwa zana na nguvukazi
Sep 09, 2025 06:57Kamanda Mkuu wa jeshi la Ukraine Aleksandr Syrsky amesema jeshi la Russia limelizidi nguvu jeshi lao katika mstari wa mbele wa vita kwa zana na nguvukazi
-
Umaarufu wa Trump nchini Marekani wakaribia kuporomoka
Sep 09, 2025 02:41Rais Donald Trump wa Marekani anaendelea kukabiliwa na hatari ya kushuka kwa kasi kwa umaarufu wake nchini humo, huku kura mbili mpya za uchunguzi wa maoni zikionyesha upinzani mkubwa wa Wamarekani dhidi ya siasa zake za kutumia wanajeshi wa Gadi ya Kitaifa kwa ajili ya kupambana na uhalifu katika miji ya Marekani.
-
Uhispania kupiga marufuku meli na ndege zinazobeba silaha za Israel
Sep 08, 2025 23:51Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, ametangaza hatua mpya kali za kidiplomasia na kiusalama zenye lengo la kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel ili usitishe mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Hatua zimepigwa katika mazungumzo na Iran
Sep 08, 2025 08:12Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameashiria hatua zilizopigwa katika mazungumzo ya kiufundi na Iran na kusema anataraji kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda siku chache zijazo na kuandaa uwanja wa kuanza tena kikamilifu ushirikiano kati ya IAEA na Tehran.
-
Kwa nini UN imetoa wito wa kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya makundi ya kutetea haki za binadamu ya Palestina?
Sep 08, 2025 05:28Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, amekosoa vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya makundi ya kutetea haki za binadamu ya Palestina, na kutoa wito wa kuondolewa mara moja.
-
Zelensky adai: Trump amempa Putin kile alichokitaka Alaska
Sep 08, 2025 04:01Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amedai kuwa Rais Donald Trump wa marekani amempatia Rais wa Russia Vladimir Putin kile alichokitaka katika mkutano wa mwezi uliopita huko Alaska.