Zelensky adai: Trump amempa Putin kile alichokitaka Alaska
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amedai kuwa Rais Donald Trump wa marekani amempatia Rais wa Russia Vladimir Putin kile alichokitaka katika mkutano wa mwezi uliopita huko Alaska.
Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa jana na ABC, Zelensky amedai kuwa Rais Putin alitamani sana kukutana na Trump.
"Alitaka sana kukutana na Rais Trump, Rais wa Marekani. Na nadhani kwamba.. Putin amepata alichokitaka, na ni huruma," amedai Rais wa Ukraine katika mahojiano hayo.
Trump, ambaye amekutana na kuzungumza na Putin mara kadhaa amekuwa akitaka kiongozi huyo wa Russia akutane ana kwa ana na Zelensky. Hata hivyo hajafanikiwa kuratibu mkutano wa aina hiyo kati ya Putin na Zelensky.
Zelansky mwigizaji aliyegeukamwanasiasa aliwahi kuzungumza mara mbili kwa simu na kukutana ana kwa ana mara mnoja na Rais Vladimir Putin mwaka 2019.
Rais huyo wa Ukraine hakualikwa kushiriki mkutano wa mwezi uliopita huko Alaska kati ya Trump na Putin.
"Inasikitisha kwamba Ukraine haikushiriki mkutano huo," amesema Zelensky.