Hatua zimepigwa katika mazungumzo na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i130558-hatua_zimepigwa_katika_mazungumzo_na_iran
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameashiria hatua zilizopigwa katika mazungumzo ya kiufundi na Iran na kusema anataraji kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda siku chache zijazo na kuandaa uwanja wa kuanza tena kikamilifu ushirikiano kati ya IAEA na Tehran.
(last modified 2025-09-08T08:12:45+00:00 )
Sep 08, 2025 08:12 UTC
  • Rafael Grossi
    Rafael Grossi

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameashiria hatua zilizopigwa katika mazungumzo ya kiufundi na Iran na kusema anataraji kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda siku chache zijazo na kuandaa uwanja wa kuanza tena kikamilifu ushirikiano kati ya IAEA na Tehran.

Rafael Grossi amesema haya wakati wa kuanza kikao cha msimu cha Bodi ya Magavana ya wakala huo mapema leo mjini Vienna, Austria. 

Grossi amesema kuwa katika wiki zilizopita walielekeza jitihada zao katika suala la kuchunguza miradi ya nyuklia ya Iran hasa baada ya mashambulio ya mwezi Juni mwaka huu. "Kama mnavyokumbuka, nimeeleza wazi suala hili na kutoa maeleo katika kikao cha Bodi ya Magavana ya IAEA na pia katika Baraza la Usalama la UN. Pia nimetoa maelezo ya kina kupitia ripoti zangu kwa Bodi ya Magavana." 

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki ameongeza kuwa: Nimekuwa nikiwasiliana mara kwa mara na Iran ili kutoa majibu kwa wasiwasi ulioibuliwa na kutafuta njia za kurejesha ushirikiano unaohitajika kati ya IAEA na Iran.

"Tumefuatilia kwa makini matukio ya karibuni ya Tehran, hususan kupasishwa sheria katika Bunge la Iran ya kusimamisha ushirikiano na wakala wa IAEA, ambayo imeidhinishwa na Rais wa Iran.