Umaarufu wa Trump nchini Marekani wakaribia kuporomoka
Rais Donald Trump wa Marekani anaendelea kukabiliwa na hatari ya kushuka kwa kasi kwa umaarufu wake nchini humo, huku kura mbili mpya za uchunguzi wa maoni zikionyesha upinzani mkubwa wa Wamarekani dhidi ya siasa zake za kutumia wanajeshi wa Gadi ya Kitaifa kwa ajili ya kupambana na uhalifu katika miji ya Marekani.
Kulingana na kura ya uchunguzi wa maoni ya CBS na U-Gov, umaarufu wa sasa wa Donald Trump ni wa asilimia 44, na katika kura ya maoni ya NBC News na Monkey Survey, umaarufu huo unaripotiwa kuwa wa asilimia 43.
Wastani wa kura za uchunguzi wa maoni za CNN kuanzia katikati ya Agosti hadi Septemba mapema pia zinaonyesha kuwa ni asilimia 43 pekee ya Wamarekani ndio wanaunga mkono utendakazi wa Trump, huku asilimia 55 wakipinga siasa zake.
Kura ya uchunguzi wa maoni ya NBC News ilifanyika kuanzia Agosti 13 hadi Septemba 1 kwa kushirikisha watu 30,196 kote Marekani ambapo kiwango cha makosa ya kura hii ni asilimia 1.9.
Kura ya uchunguzi wa maoni ya CBS ilifanyika kuanzia Septemba 3 hadi 5 kwa kushirikisha watu 2,385, na kiasi cha makosa ni asilimia 2.5.