Dabbashi akadhibisha uvumi wa kufutwa kazi UN
Jul 06, 2016 03:07 UTC
Mwakilishi wa Libya katika Umoja wa Mataifa amekadhibisha uvumi kwamba ametimuliwa kazi.
Ibrahim Omar Dabbashi amesema kuwa hakuna uamuzi wowote uliochukuliwa na Baraza la Uongozi la Libya kuhusu kumuachisha kazi.
Kituo cha habari cha African News kimeripoti kuwa, Baraza la Uongozi la Libya limemteua waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Abdur Rahman al Kiib kuwa mwakilishi wa nchi hiyo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Libya ingali inasumbuliwa na matatizo ya ndani hususan mashambulizi ya makundi ya kigaidi tangu ulipoondolewa madarakani utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Tags