Jan 11, 2024 07:47 UTC
  • Wanamgambo wa al Shabaab wauwa 1 na kuwatia nguvuni 5 kutoka helikopta ya UN

Maafisa nchini Somalia wameeleza kuwa wanamgambo wa kundi la al Shabaab wenye mfungamano na mtandao wa al Qaida jana walimuuwa mtu mmoja na kuwatekanyara wengine watano kutoka katika helikopta ya Umoja wa Mataifa huko katikati mwa Somalia.

Maafisa wa Somalia wameeleza kuwa helikopta ya Umoja wa Mataifa ilitua kwa dharura katika kijiji cha Xindheere eneo linaloshikiliwa na al Shabaab katika mkoa wa Galgudug katika jimbo la Galmudug. 

Mohamed Abdi Aden Gaboobe Waziri wa Usalama wa Ndani wa jimbo la Galmudug amesema kuwa helikopta hiyo ya Umoja wa Mataifa ilipatwa na tatizo la injini. Ameongeza kuwa, raia sita wa kigeni na Msomali mmoja walikuwa ndani ya helikopta hiyo. Gaboobe ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa wanamgambo wa al Shabaab wamewatia mbaroni abiria watano na kuumuwa mmoja ka risasi wakati akijaribu kutoroka. Hadi sasa kundi la al Shabaab halijatoa taarifa yoyote iwapo limehusika na shambulio hilo au la. 

Wanamgambo wa kitakfiri wa al Shabaab 

Afisa wa masuala ya usafiri wa anga wa Somalia ambaye hakutajwa jina lake amesema kuwa helikopta hiyo ya Umoja wa Mataifa ilikuwa ikielekea katika mji wa Wisil huko mashariki mwa Somalia kwa ajili ya uhamishaji wa kimatibabu hata hivyo lilitua kwa dharura  katika eneo linalodhibitiwa na al Shabaab.

Tags