Vikosi vya Libya vyashambulia ngome za Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11128-vikosi_vya_libya_vyashambulia_ngome_za_daesh
Vikosi vya Libya vimezishambulia ngome za wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 12, 2016 23:03 UTC
  • Vikosi vya Libya vyashambulia ngome za Daesh

Vikosi vya Libya vimezishambulia ngome za wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh kaskazini mwa nchi hiyo.

Rida Issa msemaji wa vikosi vya mji wa Misrata huko Libya amesema kuwa viwiliwili vya wanamgambo karibu 13 wa kundi la kigaidi la Daesh vimeshuhudiwa katika oparesheni hiyo. Rida Issa ameongeza kuwa mwanajeshi mmoja wa Libya ameuawa katika shambulio la makombora katika mji wa Sirte na wengine 20 kujeruhiwa.

Msemaji huyo ameongeza kuwa vikosi vyao vimeyaangamiza magari, maghala ya silaha na kuzishambulia ngome za Daesh katika mashambulizi ya anga na vifaru waliyoyafanywa dhidi ya kundi hilo. Rida Issa amesema kuwa vikosi vya jeshi vya Misrata vimeshindwa kusonga mbele kuelekea katika mji wa Sirte kufuatia mashambulizi ya kuvizia yanayofanywa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh dhidi ya vikosi hivyo. Kundi hilo lilivamia na kuyakaliwa kwa mabavu baadhi ya maeneo katika mji wa Sirte tangu mwezi Novemba mwaka juzi.