Mkutano wa UNCTAD wafunguliwa Nairobi, Kenya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11464-mkutano_wa_unctad_wafunguliwa_nairobi_kenya
Mkutano wa 14 Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD) uliofunguliwa jana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Nairobi umeanza kwa kutolewa wito wa kuwepo ushirikiano zaidi kati ya nchi za dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 18, 2016 00:33 UTC
  • Mkutano wa UNCTAD wafunguliwa Nairobi, Kenya

Mkutano wa 14 Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD) uliofunguliwa jana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Nairobi umeanza kwa kutolewa wito wa kuwepo ushirikiano zaidi kati ya nchi za dunia.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo Rais Kenyatta ametoa wito wa kuimarishwa ushirikiano wa dunia kwa ajili ya kutimiza malengo ya kijamii na kiuchumi yaliyoainishwa na nchi za dunia hususan Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG).

Rais Kenyatta alisisitizia udharira wa kuimarishwa UNCTAD ili iweze kuwa na nafasi muhimu katika kufanikisha malengo ya dunia. Amesisitzia kuwa mkutano huo ni fursa ya kubadilishana mitazamo juu ya jinsi ya kutekeleza maamuzi yanayochukuliwa na kuyaweka katika vitendo.

Mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 10,000 kutoka nchi mbalimbali duniani ambao wanafanya jitihada na kuhakikisha kwamba sera za kieneo na kimataifa zinachangia katika maendeleo endelevu. Ujumbe wa kiuchumi wa Palestina unaoongozwa na Bi Abeer Odeh, Waziri wa Uchumi wa Palestina, unashiriki katika mkutano huo ulioanza jana Jumapili jijini Nairobi.