Wahanga wa mlipuko wa lori la mafuta Nigeria wazikwa kwa umati
(last modified Thu, 17 Oct 2024 07:58:07 GMT )
Oct 17, 2024 07:58 UTC
  • Wahanga wa mlipuko wa lori la mafuta Nigeria wazikwa kwa umati

Maafisa wa serikali za mitaa kaskazini mwa Nigeria jana waliungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya maziko ya umati ya zaidi ya wahanga 140 waliopoteza maisha katika mlipuko mkubwa wa lori la mafuta usiku wa kuamkia jana.

Maafa hayo yalitokea katika mji wa Majiya katika jimbo la Jigawa kaskazini mwa Nigeria wakati lori la mafuta lililopinduka lilipowaka moto huku umati wa watu ukijaribu kukusanya mafuta yaliyokuwa yakivuja kutoka kwenye lori hilo. Mlipuko huo umesababisha uharibifu mkubwa huku aghalabu ya miili ya wahanga ikishindwa kutambuliwa. 

Maafisa husika wa Nigeria wamewatembelea baadhi ya manusura wa ajali hiyo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini. 

Matukio kama hayo ni jambo la kawaida nchini Nigeria. Mwanzoni mwa mwezi uliopita wa Septemba, makumi ya watu walipoteza maisha baada ya lori la mafuta kuripuka kaskazini mwa Nigeria. 

Milipuko ya mara kwa mara ya malori ya mafuta Nigeria

Limekuwa jambo la kawaida huko Nigeria ambapo watu wengi huhatarisha maisha yao kwa kukimbilia malori yanayopinduka ili kuchota mafuta hasa ukizingatia kupanda kwa bei ya mafuta nchini tangu serikali ilipositisha mpango wake wenye gharama kubwa wa kufadhili ruzuku ya gesi.

Tags