Libya ina hamu ya kujiunga na BRICS
Libya imetangaza kuwa ina hamu ya kujiunga na jumuiya ya uchumi ya BRICS. Hayo yameelezwa na afisa wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo.
Kaimu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Umoja wa Taifa ya Libya Taher al-Bawr amesema katika mahojiano na TASS kando ya Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Russia na Afrika.
Taher al-Bawr amesema: "tuna nia ya kujiunga, lakini kujiunga ni hakikisho la thamani, faida ambayo Libya inaweza kupata kwa kujiunga na jumuiya. Kimsingi, kwa sasa tunatalii uwezekano wa kujiunga na BRICS katika duru za serikali. Na vile vile suala hili linahitaji utafiti wa kina zaidi na tathmini ya manufaa ambayo Libya itapata kutokana na kujiunga na kundi la BRICS".
Kuhusiana na mkutano wa BRICS uliofanyika nchini Russia, mwanadiplomsia huyo wa Libya amesema: "kwa bahati mbaya, hatukualikwa hata kwenye mkutano uliopita wa BRICS, ingawa tulitaka kuhudhuria angalau kujifunza zaidi kuhusu fursa zinazotolewa na jumuiya hiyo".