Utafiti mpya: Idadi ya waliouawa vitani Sudan inaweza kuwa ya juu zaidi
(last modified Fri, 15 Nov 2024 03:54:12 GMT )
Nov 15, 2024 03:54 UTC
  • Utafiti mpya: Idadi ya  waliouawa vitani Sudan inaweza kuwa ya juu zaidi

Zaidi ya watu 61,000 wanakadiriwa kupoteza maisha katika jimbo la Khartoum katika kipindi cha miezi 14 ya kwanza ya vita vya Sudan. Ushahidi unaonyesha kuwa idadi ya watu waliouliwa vitani ni kubwa zaidi kuliko ilivyosajiliwa hapo awali. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya watafiti nchini Uingereza na Sudan.

Makadirio hayo yanajumuisha watu wapatao 26,000 waliokabiliwa na vifo vya kikatili huko Sudan; idadi  ambayo ni kubwa kuliko ile iliyoripotiwa na Umoja wa Mataifa. 

Utafiti wa awali uliofanywa ulionyesha kuwa kuwa njaa na magonjwa yanaendelea kuwa sababu kuu za vifo kote Sudan.

Wakati huo huo uchunguzi wa watafiti wa Uingereza na Sudan unaonyesha kuwa kiwango cha makadirio ya vifo vilivyosababishwa sababu zote katika jimbo la Khartoum vilikuwa  vya asilimia 50 kabla ya kuanza mapigano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) mwezi Aprili 2023.

Jeshi la Sudan linalopigana na kikosi cha RSF

Umoja wa Mataifa kwa upande wake umeeleza kuwa vita vya Sudan vimepelekea watu milioni 11 kuhama makazi yao na baadhi yao kukimbilia katika nchi jirani. Aidha watu karibu milioni 25 yaani nusu ya jamii nzima ya watu wa Sudan wanahitaji misaada ya kibinadamu hasa chakula kufuatia kuathiriwa na njaa jamii khususan wakimbizi walioko makambini.