Polisi Afrika Kusini wavamia maghala ya chakula kusaka bidhaa zilizokwisha muda wake
(last modified Fri, 22 Nov 2024 02:32:16 GMT )
Nov 22, 2024 02:32 UTC
  • Polisi Afrika Kusini wavamia maghala ya chakula kusaka bidhaa zilizokwisha muda wake

Polisi wa Afrika Kusini wamegundua vyakula vinavyoshukiwa kuisha muda wake wakati walipovamia maghala kadhaa ya chakula mjini Durban.

Haya yanajiri huku mamlaka husika za Afrika Kusini zikijaribu kuzuia matukio kadhaa ya ulaji wa vyakula vinavyoshukiwa kuwa vibofu na visivyofaa kutumiwa na binadamu ambayo vimesababisha  vifo vya watoto wasiopungua 20, wengi wao wakiwa wanafunzi, katika wiki za hivi karibuni.

Nhlanla Mkhwanazi, Kamishna wa Polisi ya Afrika Kusini ameongoza timu ya maafisa wa polisi kukagua stoo hizo zilizokuwa zimehifadhi bidhaa mbalimbali za chakula katika mji wa Durban. 

Polisi wa Afrika Kusini wamefanikiwa kunasa maghala mawili ya chakula kinachodaiwa kumalizika muda wake pamoja na dawa kadhaa za matibabu. 

Waligundua kwa uchache maghala mawili yanayodaiwa kuhifadhi vyakula vilivyopitwa na wakati na dawa zza matibabu ya binadamu.

''Tunahitaji kujua ni nani anayeleta bidhaa hizi, anazipeleka wapi, anauza kwa nani, na mwisho wake ni wapi?” amesema Kamishna wa Polisi ya Afrika Kusini.