Wafanyabiashara Nigeria wataka kususiwa bidhaa za Israel
Kundi moja la wajasiriamali wadogo na wa kati nchini Nigeria, limeandaa mkutano wa siku mbili katika Jimbo la Kaduna la kaskazini magharibi mwa nchi, kujadili mikakati ya kibiashara na umuhimu wa kususia bidhaa za Israel, ili kuonyesha uungaji mkono kwa kadhia ya Palestina.
Mkutano huo umeandaliwa na kundi la "Filin 'Yar Kwalisa" ambayo ina maana ya kupamba na kuchagiza maisha. Kundi hilo ni jukwaa linalojumuisha wafanyabiashara, wasomi, na wajasiriamali kutoka Kaskazini mwa Nigeria ambao kila mwaka huandaa makongamano ili kuimarisha biashara zao.
Sumayya Abubakar Makki, mfanyabiashara kutoka Jimbo la Bauchi anayeshiriki mkutano huo amesema, "Kama wafuasi wa Mhimili wa Muqawama, lazima tujiweka mbali na bidhaa zote za Israel na kutafuta njia mbadala kutoka kwa nchi zinazoupinga utawala wa Israel."
Naye Zainab Muhammad, mhitimu wa uuguzi ambaye pia amehudhuria kongamano hilo, ameashiria bidhaa zenye ubora wa juu kutoka Iran, na kupongeza mihadhara ya mkutano huo iliyojadili mikakati ya biashara, na umuhimu wa kuepuka bidhaa zinazosaidia uchumi wa Israel.

Utawala haramu wa Israel unakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi kutokana na hatua za kimataifa za kususia bidhaa na huduma zinazotolewa na utawala huo mtenda jinai.
Katika barua ya wazi, wachumi 300 wa Israel walionya hivi karibuni kuwa, kususiwa Israel kunaenda zaidi ya kutonunua baadhi ya bidhaa za utawala huo wa Kizayuni.