Joto lasababisha madhara makubwa barani Afrika
(last modified Tue, 13 May 2025 12:24:34 GMT )
May 13, 2025 12:24 UTC
  • Joto lasababisha madhara makubwa barani Afrika

Ripoti mpya kuhusu “Hali ya Hewa Afrika 2024” iliyotolewa wiki hii na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO imeonya kwamba muongo wa joto zaidi kuwahi kushuhudiwa Afrika umeleta madhara makubwa kwa bara hilo.

Katika ripoti hiyo iliyotolewa mjini Addi Ababa na Geneva WMO imesema “Afrika imeshuhudia muongo wa joto zaidi katika historia, huku joto kali, mawimbi ya joto baharini yasiyokuwa ya kawaida, mafuriko na ukame unaoangamiza maisha ya watu vikizidi kuongezeka kote barani humo”.

Katibu Mkuu wa WMO, Celeste Saulo amesema "Ripoti ya Hali ya Hewa Afrika inaonesha uharaka na uhalisia unaoongezeka wa mabadiliko ya tabianchi barani humo. Tunaona mwelekeo wa wazi wa matukio ya hali mbaya ya hewa yanayotishia maisha, kipato, na uchumi."

Mwaka 2024, kwa mujibu wa ripoti Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ilikumbwa na ukame mbaya zaidi katika angalau miongo miwili, huku nchi kama Zambia na Zimbabwe zikishuhudia kupungua kwa mavuno ya nafaka kwa asilimia 43 Zambia na asilimia 50 Zimbabwe chini ya wastani wa miaka mitano.

Wakati huo huo, Afrika Mashariki ilipata mafuriko mabaya yaliyowafurusha zaidi ya watu 700,000 na kuua mamia nchini Kenya, Tanzania, na Burundi.

Dkt. Mary Kambona, mtaalamu wa tabianchi wa Kikanda amesema “Tunapambana na majanga kwa pande zote mbili, maeneo mengine yamekauka wakati mengine yanafurika. Hili ni janga la kibinadamu na la maendeleo kwa wakati mmoja."

Ripoti hiyo ya WMO imezihimiza serikali, washirika wa maendeleo, na sekta binafsi kuharakisha uwekezaji wa tabianchi unaozingatia ujasiri na kupanua wigo wa mifumo ya tahadhari za mapema kote barani Afrika.