OCHA: Mamilioni Sahel Afrika wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i127302-ocha_mamilioni_sahel_afrika_wanahitaji_msaada_wa_haraka_wa_kibinadamu
Mamilioni ya watu katika Ukanda wa Sahel Afrika wanahitajia msaada wa haraka wa kibinadamu na hali yao inatarajiwa kuuwa mbaya zaidi katika siku zijazo kama misaada hiyo haitafikishwa kwa wakati.
(last modified 2025-06-08T00:16:21+00:00 )
Jun 08, 2025 00:16 UTC
  • OCHA: Mamilioni Sahel Afrika wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu

Mamilioni ya watu katika Ukanda wa Sahel Afrika wanahitajia msaada wa haraka wa kibinadamu na hali yao inatarajiwa kuuwa mbaya zaidi katika siku zijazo kama misaada hiyo haitafikishwa kwa wakati.

Takriban watu milioni 29 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu na ulinzi katika ukanda wa Sahel. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa wiki hii na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).

Utafiti huo unahusu Burkina Faso, Chad, Mali, Niger, pamoja na kaskazini ya mbali ya Cameroon na kaskazini mashariki mwa Nigeria. Shirika hilo linatoa wito kwa wafadhili, likionya kwamba bila ufadhili unaohitajika, maisha ya mamilioni ya watu yatakuwa hatarini.

Kulingana na OCHA, takwimu zimeongezeka kwa 6% na 20% mtawalia tangu mwanzoni mwa mwaka 2024: Sahel sasa ina wakimbizi milioni 2 na wakimbizi wa ndani milioni 6.

Kukimbia huku kwa watu kunahusishwa na migogoro mbalimbali iliyoingiliana, ukosefu wa usalama, umaskini, kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, na matokeo ya mabadiliko ya tabianchi, miongoni mwa mengine.

Kati ya mwezi Juni na mwezi, OCHA inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 12 watakabiliwa na uhaba wa chakula katika eneo la Sahel.

Mwaka jana, matukio mengi ya uukosefu wa usalama yalitokea katika Sahel ya Kati na Bonde la Ziwa Chad. Matukio hayo yalisababisha karibu vifo 17,000 na kupelekea kufungwa kwa takriban vituo 1,000 vya afya na karibu shule 10,000-zaidi ya nusu yao ziko Burkina Faso.