Sudan yamtuhumu Haftar kwa kuunga mkono wanamgambo wa RSF
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imemtuhumu Khalifa Haftar mbabe wa kivita wa Libya kwa kuunga mkono mashambulizi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan na Wizara ya Mashauri ya Kigeni vimemtuhumu Jenerali mstaafu wa Libya Khalifa Haftar kwa kuunga mkono shambulio lililoanzishwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka kwenye vituo vya mpaka katika pembetatu ya mpaka wa Sudan-Misri-Libya. Kwa mujibu wa taarifa ya Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan, Vikosi vya Msaada wa Haraka, vikiungwa mkono na Kikosi cha Haftar cha Kisalafi, vilishambulia maeneo ya mpaka katika pembe tatu ya mpaka wa Sudan-Misri-Libya, kwa lengo la kuteka eneo hilo la kimkakati.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, uingiliaji kati huu wa moja kwa moja wa vikosi vya Haftar ni "ukiukaji wa wazi" wa mamlaka ya Sudan na watu wake, na kubainisha kuwa, shambulio hilo ni sehemu ya njama za kimataifa na kikanda mbele ya macho jamii ya kimataifa.
Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imetoa taarifa ikilaani shambulio hilo na kulitaka kuwa, "ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa," na kubainisha kwamba, ushiriki wa Brigedi ya Kisalafi katika shambulio ndani ya ardhi ya Sudan ni "kuongezeka hatari ya uchokozi wa nje unaoungwa mkono na serikali ya Imarati