Dira ya 2050 kuigeuza Tanzania nchi ya Uchumi wa $Trilioni 1
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Julai 17 imezindua rasmi Dira ya Taifa ya 2050 katika hafla maalumu iliyohudhuriwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa Dira hiyo, nchi hiyo ya Afrika Mashariki imejiwekea lengo la kufikia uchumi wa dola za Marekani trilioni 1 ikitoka kwenye uchumi wa dola bilioni 85.42 mwaka 2024 na vilevile kupandisha kipato cha kila mtu hadi dola 7,000 kutoka dola 1,277 mwaka 2023.
Duru za masuala ya kiuchumi za nchi hiyo zinasema, hadi sasa taifa hilo limepiga hatua kupitia ukuaji wa uchumi wa wastani wa 6.2% kwa mwaka, kupunguza umasikini uliokithiri kutoka 36% hadi 26% na kuboresha sekta muhimu kama kilimo na miundombinu. Hata hivyo, changamoto bado ni kubwa, kutokana na idadi ya watu kutarajiwa kuongezeka hadi milioni 140 wakati huo, hali itakayoongeza mahitaji ya ajira, elimu na huduma za afya.
Imeelezwa pia kwamba, changamoto za miundombinu, mabadiliko ya taibianchi na matatizo ya utawala kama rushwa na ukosefu wa uwazi wa kisheria vingali vinazuia kasi ya maendeleo…/