Wagombea 81 wachukua fomu ya kuwania kiti cha urais Cameroon
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i128630-wagombea_81_wachukua_fomu_ya_kuwania_kiti_cha_urais_cameroon
Jumla ya wagombea 81 wamejaza fomu na kuwasilisha kwa Tume ta Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi wa Rais wa Oktoba mwaka huu.
(last modified 2025-07-22T14:09:27+00:00 )
Jul 22, 2025 14:09 UTC
  • Wagombea 81 wachukua fomu ya kuwania kiti cha urais Cameroon

Jumla ya wagombea 81 wamejaza fomu na kuwasilisha kwa Tume ta Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi wa Rais wa Oktoba mwaka huu.

Bello Bouba Maigari anagombea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais wa Cameroon kwa mara ya pili katika harakati zake za kisiasa baada ya kuacha kumuunga mkono Rais wa nchi hiyo Paul Biya mapema mwaka huu. 

Hali hii ya mambo inashuhudiwa pia kwa Maurice Kamto na Cabral Libii wagombea wawili ambao wamebadilisha msimamo wa kisiasa wa vyama vyao kwa kuamua kugombea kiti cha urais mwaka huu. 

Wimbi hili kubwa la maombi wagombea wa kiti cha urais nchini Cameroon katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu linadhibitiwa na wanaume. Ni wanawake saba tu waliotangaza nia ya kugombea kiti cha urais kati ya jumla ya maombi 81 yaliyowasilishwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo. 

Rais wa Cameroon Paul Biya ambaye amedumu madarakani kwa muda mrefu barani Afrika anaongoza katika orodha hiyo ya majina ya wagombea 81 wa kiti cha urais mwaka huu. 

Rais Paul Biya wa Cameroon

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 92, ambaye amekuwa madarakani kwa miongo minne sasa, hivi karibuni alitangaza nia yake ya kuwania tena wadhifa huo licha ya wasiwasi mkubwa juu ya afya na uwezo wake wa kuongoza nchi.