Algeria yahimiza kuachiwa huru raia wake wote walioko jela Guantanamo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i13780-algeria_yahimiza_kuachiwa_huru_raia_wake_wote_walioko_jela_guantanamo
Waziri wa Sheria wa Algeria amesisitiza juu ya udhaura wa kuachiwa huru raia wote wa nchi hiyo waliofungwa katika jela ya Guantanamo nchini Cuba.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 22, 2016 23:38 UTC
  • Algeria yahimiza  kuachiwa huru raia wake wote walioko jela Guantanamo

Waziri wa Sheria wa Algeria amesisitiza juu ya udhaura wa kuachiwa huru raia wote wa nchi hiyo waliofungwa katika jela ya Guantanamo nchini Cuba.

Tayeb Louh, amesema raia wawili wa nchi hiyo wamefungwa katika jela ya Guantanamo na kusisitiza kuwa raia hao pia kama walivyo wafungwa wengine wanapasa kukabidhiwa kwa serikali ya Algiers.

Tayeb Louh ameongeza kuwa suala la raia wa Algeria walioko jela huko Guantanamo lina umuhimu mkubwa kwa serikali ya Algeria na kwamba nchi hiyo inafuatilia kwa makini suala hilo.  Hadi kufikia sasa maafisa wa Marekani wamewaachia huru raia18 wa Algeria waliokuwa wamefungwa jela huko Guantanamo. Hii ni katika hali ambayo raia wengine 61 wa mataifa mbalimbali wanatumikia kifungo huko Guantanamo huku wakikabiliwa na hali mbaya ndani ya jela.  Jela ya Guantanamo huko Cuba iliasisiwa wakati wa utawala wa Rais wa zamani wa Marekani  George W. Bush; ambapo wafungwa wamekuwa wakiteswa na kunyanyaswa vikali kwa njia mbalimbali kama kumwagiwa maji mfungwa huku uso na kichwa kikiwa kimefunikwa na kutishiwa mbwa. 

Mfungwa katika jela ya Guantanamo akitishiwa mbwa

Rais Barack Obama wa Marekani tarehe 22 mwezi Januari mwaka 2009 aliahidi baada ya kushinda uchaguzi kuwa katika muda wa mwaka mmoja ataifunga jela ya Guantanamo, hata hivyo hadi sasa Obama ameshindwa kutekeleza ahadi yake hiyo.