Wananchi wa Mali waandamana kumuunga mkono kiongozi wao wa kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i138280-wananchi_wa_mali_waandamana_kumuunga_mkono_kiongozi_wao_wa_kijeshi
Mamia ya waungaji mkono wa uongozi wa serikali ya kijeshi ya Mali Jumamosi walijumuika katika uwanja wa michezo katika mji mkuu, Bamako ili kuthibitisha uungaji mkono wao kwa serikali ya mpito ya nchi hiyo.
(last modified 2026-05-10T10:18:52+00:00 )
May 10, 2026 10:09 UTC
  • Wananchi wa Mali mjini Bamako
    Wananchi wa Mali mjini Bamako

Mamia ya waungaji mkono wa uongozi wa serikali ya kijeshi ya Mali Jumamosi walijumuika katika uwanja wa michezo katika mji mkuu, Bamako ili kuthibitisha uungaji mkono wao kwa serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Wananchi wa Mali walijumuika mjini Bamako kufuatia wito wa serikali ya mpito ya nchi hiyo ambayo imekuwa madarakani tangu mwaka 2020 huku ikikabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha.

Wananchi wa Mali kwa mara nyingine tena wametangaza uungaji mkono wao kwa serikali kufuatia mashambulizi yaliyoratibiwa na makundi ya waasi mwezi uliopita ambayo yalisababisha vifo vya watu kadhaa, akiwemo Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Sadio Camara. 

Aprili 26 Mali ilikkabiliwa na moja ya mashambulizi makubwa zaidi ya makundi yenye silaha dhidi ya jeshi la nchi hiyo katika mji mkuu, Bamako na miji mingine kadhaa.