Wanachama wanne wa Daesh watiwa mbaroni Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14692-wanachama_wanne_wa_daesh_watiwa_mbaroni_somalia
Wanachama wanne wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wametiwa mbaroni kusini mwa Somalia.
(last modified 2025-11-19T08:00:07+00:00 )
Sep 05, 2016 14:02 UTC
  • Wanachama wanne wa  Daesh watiwa mbaroni Somalia

Wanachama wanne wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wametiwa mbaroni kusini mwa Somalia.

Askari usalama wa Somalia wamewatia mbaroni wanachama wanne wa kundi la kigaidi la Daesh kufuatia oparesheni waliyofanya katika mji wa Baidoa kusini mwa nchi hiyo. Mohamed Isla Aflow Mkuu wa Kitengo cha  Intelijinsia na Usalama kusini mwa Somalia ameeleza kuwa Abdulkadir Mumin kiongozi wa masuala ya kijeshi wa Daesh katika eneo ni miongoni mwa wanachama hao wanne wa Daesh waliokamatwa huko Baidoa. Aflow ameongeza kuwa kinara huyo alikuwa akilitumikia kundi la Daesh ambap alitaraji kusimamia oparesheni ya uharibifu ya kundi hilo katika eneo la Bay kusini mwa Somalia.

Abdulkadir Mumin kiongozi wa Daesh nchini Somalia aliyekamatwa na vikosi vya Somalia

Wanachama hao wanne wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wametiwa mbaroni siku moja baada ya Marekani kuliweka katika orodha ya magaidi wa mashariki mwa Afrika jina la Abdulkadir Mumin kiongozi wa kundi la Daesh huko Somalia.