Ki-moon asisitiza kulindwa umoja wa kisiasa Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14833-ki_moon_asisitiza_kulindwa_umoja_wa_kisiasa_kongo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyatolea wito makundi yanayozozana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kulinda umoja wa kisiasa na kujiunga na mchakato wa mazungumzo ya kitaifa ili nchi hiyo irejee katika hali ya amani na utulivu.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 07, 2016 09:25 UTC
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyatolea wito makundi yanayozozana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kulinda umoja wa kisiasa na kujiunga na mchakato wa mazungumzo ya kitaifa ili nchi hiyo irejee katika hali ya amani na utulivu.

Ban Ki-moon amesema leo kuwa njia pekee ya kurejesha amani na uthabiti huko Kongo ni kwa makundi yanayozozana nchini humo kujiunga na mchakato mpya wa mazungumzo ya kitaifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amebainisha kuwa kufanyika mazungumzo mapana ya kisiasa huko Kongo kutasaidia kuandaa uwanja wa kufanyika uchaguzi wenye itibari.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia ameashiria mchakato mpya wa mazungumzo ya kitaifa ya Kongo yaliyoanza tangu tarehe Mosi Septemba mwaka huu na kueleza kuwa, serikali inapasa kuendeleza hatua za kujenga hali ya kuaminiana ili kuandaa anga nzuri ya kusogeza mbele mazungumzo ya kitaifa kwa  kutekelezwa haki na uhuru uliosisitizwa kwenye katiba ya Kongo. 

Baadhi ya washiriki wa mazungumzo ya kitaifa ya Kongo DR

Mchakato mpya wa mazungumzo ya kitaifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa shabaha ya kuzuia kuibuka mivutano ya kisiasa yalianza wiki iliyopita .