Sep 11, 2016 04:34 UTC
  • Jeshi la Nigeria: Tumeazimia kurejesha usalama eneo la Niger Delta

Jeshi ya Nigeria limetangaza kuwa, licha ya kushadidi mashambulizi ya waasi wa Ulipizaji Kisasi katika eneo la Niger Delta kusini mwa nchi hiyo, lakini limeazimia kurejesha usalama ana amani eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imesema kuwa, kupitia operesheni zilizopewa jina la 'Tabasamu ya Mamba' askari wa serikali wamefanikiwa kusambaratisha vituo 74 vya uzalishaji na uuzaji mafuta ya magendo, mali ya waasi hao. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kikosi maalumu cha mapambano kimeandaliwa tayari kwa ajili ya kutekeleza operesheni dhidi ya waasi wa Niger Delta.

Wapiganaji wa Niger Delta

Mashambulizi ya makundi ya wabeba silaha katika eneo hilo lenye utajiri wa mafuta kusini mwa taifa hilo la magharibi mwa Afrika, yameshadidi suala lililoifanya serikali kutoa indhari kali eneo lililotajwa. Ujumbe uliotolewa na waasi hao kwa Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo ulisema kuwa, hatua chanya na za kiuadilifu za serikali zinaweza kurejesha usalama sanjari na usitishaji machafuko. Aidha ujumbe huo sanjari na kutangaza utayarifu wao kwa ajili ya kufanya mazungumzo na serikali, ulisema kuwa hatua ya Rais Buhari ya kupeleka askari eneo la Niger Delta haitakuwa na natija yoyote. 

Tags