Sep 29, 2016 04:39 UTC
  • Vijana kadhaa wa Chad warejea nchini kutoka katika kambi za Boko Haram

Duru za kuaminika zimearifu habari ya kurejea nchini vijana kadhaa wa Chad kutoka katika kambi za wanamgambo wa kundi la Boko Haram huko Nigeria.

Duru za kuamiminika nchini Chad zimeeleza kuwa raia 60 wakiwemo wanawake watatu na vijana wakazi wa eneo la Lac magharibi mwa Chad karibu na mpaka wa Nigeria ambao walikuwa wanachama wa Boko Haram,  wiki iliyopita waliondoka katika mojawapo ya kambi za kundi hilo na kurudi Chad. Eneo la Lac linatambuliwa kama lango linalotumiwa na Boko Haram kuingilia Chad. Adoum Forteil Gavana wa eneo la Lac amewahahakishia wakazi wa eneo hilo kuwa wanachama hao walioachana na  kundi la Boko Haram watakuwa chini wa uangalizi. Kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram  limekuwa likitenda hujuma na mashambulizi huko Nigeria tangu mwaka 2009, na mwaka jana kundi hilo lilianza kutekeleza mashambulizi huko Niger,Cameroon na Chad.

Nchi nne ambazo zimekuwa zikilengwa na mashambulizi ya Boko Haram

Watu wanaokaribia elfu ishirini wameuawa na wengine milioni mbili na laki sita wamebaki bila ya makazi kufuatia mashambulizi ya Boko Haram.  

Tags