Rwanda yataka wakimbizi wa Burundi waondoke
Feb 24, 2016 07:09 UTC
Rwanda imesema ni lazima wakimbizi wa Burundi walioko kwenye nchi hiyo wahamishiwe kwenye nchi ya tatu.
Rwanda inasema inafanya hivyo kuepuka
kuendelea kuchafuliwa jina lake kutokana na kile inachokitaja kama
propaganda za serikali ya Burundi kulifanya suala la wakimbizi kama la
kisiasa. Burundi imekuwa ikilaumu Rwanda kuwapa silaha na mafunzo
wakimbizi wa Burundi suala ambalo Rwanda imekuwa ikilikanusha.
Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.
Tags