Rais Museveni apongeza uhusiano mzuri wa Uganda na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21415-rais_museveni_apongeza_uhusiano_mzuri_wa_uganda_na_iran
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amepokea vitambulisho vya balozi mpya wa Iran nchini humo na kupongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya Tehran na Kampala.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 14, 2016 10:41 UTC
  • Rais Museveni apongeza uhusiano mzuri wa Uganda na Iran

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amepokea vitambulisho vya balozi mpya wa Iran nchini humo na kupongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya Tehran na Kampala.

Akizungumza wakati akipokea vitambulisho vya Sayyed Morteza Mortazavi Balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uganda mapema leo Jumatano, Rais Museveni amesema hakuna vizingiti vyovyote katika kustawishwa uhusiano wa nchi hizi mbili katika nyanja mbali mbali

Rais Museveni ameongeza kuwa, Uganda inakaribisha ushirikiano wowote ule na mashirika ya Kiirani hasa katika zekta za kilimo, viwanda vya vyakula, sekta ya madini, ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme na biashara baina ya nchi mbili.

Rais Museveni

Rais Museveni ameashiria kumbukumbu yake kuhusu zama za kupambana na diktetea aliyepinduliwa Uganda na kusema kipindi hicho kilisadifiana na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Amesema katika kipindi hicho mataifa mawili ya Iran na Uganda yalikuwa yakipambana na pale Mapinduzi ya Kiislamu yaliyopata ushindi, jambo hilo lilikuwa ni motisha kwa wanamapambano wa Uganda.

Kwa upande wake Balozi Mortazavi amemtaja Rais Museveni kuwa mwanamapambano, mwenye misimamo huru, mwanafikra na kiongozi anayependwa na wananchi. Aidha amemshukuru kwa jitihada zake za kuimarisha uhusiano wa nchi mbili.