Waliojaribu kuingiza bomu kambi ya GSU Kenya wakamatwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2323-waliojaribu_kuingiza_bomu_kambi_ya_gsu_kenya_wakamatwa
Vyombo vya usalama nchini Kenya vimesema vinawashikilia watu wawili akiwemo afisa wa zamani wa polisi kwa tuhuma za kujaribu kuingiza bomu kwenye kambi ya polisi wa kuzima fujo (GSU) wakati wa hafla za mahafali ambapo Rais Uhuru Kenyatta ndiye aliyekuwa mgeni wa heshima.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 02, 2016 23:37 UTC
  • Waliojaribu kuingiza bomu kambi ya GSU Kenya wakamatwa

Vyombo vya usalama nchini Kenya vimesema vinawashikilia watu wawili akiwemo afisa wa zamani wa polisi kwa tuhuma za kujaribu kuingiza bomu kwenye kambi ya polisi wa kuzima fujo (GSU) wakati wa hafla za mahafali ambapo Rais Uhuru Kenyatta ndiye aliyekuwa mgeni wa heshima.

Habari zinasema afisa wa zamani wa polisi alikamatwa akiwa na mada za milipuko nje ya lango la chuo cha mafunzo cha GSU katika eneo la Embakasi, viungani mwa jiji la Nairobi na kisha kuzuiliwa na walinda usalama. Washukiwa hao wanashikiliwa katika makao makuu ya kitengo cha polisi cha kupambana na ugaidi. Habari zinasema wawili hao walikutwa na vifaa na mada ambazo zikiwekwa pamoja zinaweza kuunda bomu lenye nguvu.

Jaribio hilo la kuingiza bomu katika eneo alilokuwa rais wa Kenya limefanyika siku chache baada ya kundi la kigaidi la al-Shabab kutoa vitisho vya kushambulia maeneo muhimu ya nchi hiyo vikiwemo viwanja vya ndege.