Jammeh apewa muhula aondoke Gambia la sivyo majeshi ya kigeni yatamtimua
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i23944-jammeh_apewa_muhula_aondoke_gambia_la_sivyo_majeshi_ya_kigeni_yatamtimua
Wanajeshi wa nchi za Afrika Maghairbi wamesimamisha operesheni yao ya kumuondoa madarakani Rais Yahya Jammeh wa Gambia na kumpa fursa ya kuondoka kwa heshima kupitia mazungumzo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 20, 2017 04:06 UTC
  • Rais Yahya Jammeh wa Gambia
    Rais Yahya Jammeh wa Gambia

Wanajeshi wa nchi za Afrika Maghairbi wamesimamisha operesheni yao ya kumuondoa madarakani Rais Yahya Jammeh wa Gambia na kumpa fursa ya kuondoka kwa heshima kupitia mazungumzo.

Leo Ijumaa Rais Alpha Conde wa Guinea anatazamiwa kufanya ziara nchi Gambia kwa minajili ya kumshawishi Yahya Jammeh akabidhi madaraka.

Jaribio la mwisho katika kumshawishi Yahya Jammeh kuachia ngazi kwa amani litafanyika leo Ijumaa, Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS Alain Marcel de Souza amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dakar, Senegal na kuongeza kuwa:  "Kama saa sita mchana, atakua bado hajakubali kuondoka nchini chini jitihada za Profesa Alpha Conde, askari wataingilia kijeshi na kumuondoa madarakani kwa nguvu." Wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi tayari wako Gambia wakisubiri amri ya kuingia mji mkuu Banjul kumtimua Jammeh akikataa kuondoka.

Adama Barrow akiapishwa jana huko Dakar, Senegal

Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow, hatimaye aliapishwa rasmi kuwa rais wa nchi hiyo katika ofisi za ubalozi wa Gambia zilizoko jijini Dakar, Senegal jana Alkhamisi, na kutoa mwito kwa wanajeshi kuonesha utiifu kwa Serikali yake.

Barrow, amelazimika kuapishwa nje ya nchi yake kutokana na kuhofia usalama wake pamoja na hatua ya Rais Yahya Jammeh kukataa kuondoka madarakani, akipinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi Disemba mwaka jana huko Senegal.