Makubaliano ya kusitisha mapigano yafikiwa nchini Libya
Baraza la Uongozi la Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya limetangaza kuwa, kumefikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.
Baraza la Uongozi la Libya limeashiria makubaliano ya kusitisha vita nchjini humo na kutangaza kuwa, kumeundwa kamati ya kiusalama kwa ajili ya kufuatilian utekelezwaji wa makubaliano hayo na vile vile kamati kutoka Wiazara ya Afya ambayo itakuwa na jukumu la kufuatilia matibabu ya majeruhi huku kukiwa na kamati nyingine ambayo yenyewe itatathmini hasara dhidi ya majengo na kuzilipa fidia familia na watu waliodhurika.
Taarifa hiyo imeitaka jamii ya kimataifa pia itekeleze majukumu yake ipasavyo kuhusiana na usalama wa raia wa Libya na kuunga mkono amani na uthabiti katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Aidha imetoa wito wa kusaidiwa Libya katika kulipatia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa usalama na kuwafuatilia kisheria watu wanaovuruga amani na uthabiti wa nchi hiyo.
Baraza la Uongozi la Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya limesisitiza pia juu ya azma yake ya kuendeleza juhudi zake za kupambana na aina yoyote ile ya umiliki wa silaha kinyume cha sheria.
Alkhamisi iliyopita mji mkuu Tripoli ulishuhudia mapigano ya hapa na pale baina ya vikosi vya usalama vya makao makuu tawi la Abu Salim linalofungamana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya pamoja na brigedi inayofungamana na Wizara ya Ulinzi ya Setrikali ya Wokovu wa Kitaifa ambapo watu kadhaa waliuawa na kujeruhiwa.