UN yatahadharisha kuhusu hali ya wakimbizi wanawake na watoto nchini Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25756-un_yatahadharisha_kuhusu_hali_ya_wakimbizi_wanawake_na_watoto_nchini_libya
Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya wakimbizi wanawake na watoto katika kambi za wakimbizi zilizoko nchini Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 28, 2017 12:45 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu hali ya wakimbizi wanawake na watoto nchini Libya

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya wakimbizi wanawake na watoto katika kambi za wakimbizi zilizoko nchini Libya.

Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeripoti kuwa, wanawake na watoto wanaoelekea Ulaya kupitia njia hatari ya baharini wakikimbia umaskini na vita barani Afrika wanalazimika kuishi katika kambi zenye hali mbaya kupita kiasi nchini Libya au kukabiliana na ubakaji, njaa na mauadhi ya aina mbalimbali. 

Wakimbizi katika kambi nchini Libya

UNCEF imeripoti kuwa, makundi yenye silaha nchini Libya yanadhibiti vituo rasmi vya kuhifadhia wakimbizi na yanashirikiana na magenge ya wahalifu na wafanya magendo ya binadamu. Ripoti hiyo imeongeza kuwa nusu ya wakimbizi waliohojiwa katika vituo hivyo vilivyoko nchini Libya wamesema kuwa wamebakwa na kunajisiwa mara kadhaa.

Mkurugenzi wa Kanda wa UNICEF, Afshan Khan amesisitiza udharura wa kupunguzwa kasi ya uhajiri duniani na kufanyika jitihada za kutayarishwa mazingira bora zaidi kwa watoto wakimbizi.

Afshan Khan

Afshan Khan amesema maisha ya watoto hayapasi kuachwa mikononi mwa wafanya magendo ya binadamu kutokana na ukosefu wa taratibu za kisheria za kushughulikia hali yao.