Mar 16, 2017 14:34 UTC
  • Sudan Kusini: Marekani inachochea machafuko kwa kuwafadhili waasi nchini mwetu

Serikali ya Juba imeituhumu Marekani kuwa inachochea machafuko na mapigano nchini humo, kwa kuyaunga mkono na kuyafadhili magenge ya waasi.

Vyombo vya habari nchini Sudan Kusini vimeripoti kuwa, Shirika Kuu la Kijasusi la Marekani (CIA) linaunga mkono na kulizatiti kwa silaha kundi jipya la waasi linaloongozwa na aliyekuwa Naibu Mkuu wa Jeshi katika nchi hiyo changa zaidi barani Afrika, Jenerali Thomas Cirilo Swaka.

Jenerali Cirilo ameyaleta pamoja magenge kadhaa ya waasi nchini Sudan Kusini, ambayo yameshadidisha mapigano nchini humo katika siku za hivi karibuni, kwa lengo la kumuondoa mamlakani Rais Salva Kiir.

Magenge ya waasi Sudan Kusini

Mwishoni mwa mwaka uliopita baada ya Washington kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Sudan Kusini, Makamu wa Rais wa nchi hiyo ya Kiafrika, Taban Deng Gai aliilaumu Marekani kwa siasa zake zisizo sahihi kuhusiana na nchi hiyo na kusema kuwa, Juba inahitajia misaada ya kila namna na si vikwazo. 

Mwezi Novemba mwaka jana mtaalamu wa Umoja wa Mataifa alionya kuwa, yumkini Sudan Kusini ikatumbukia katika mauaji ya kimbari kutokana na kushadidi mapigano ya kikabila baina ya makundi mengi hasimu nchini humo.

Tags