UN yatahadharisha kuhusu hatari za maharamia wa Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i27344-un_yatahadharisha_kuhusu_hatari_za_maharamia_wa_somalia
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na mihadarati na uhalifu ametahadharisha kuhusu hatari, vitisho na mashambulizi ya maharamia wa baharini nchini Somalia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 05, 2017 22:48 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu hatari za maharamia wa Somalia

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na mihadarati na uhalifu ametahadharisha kuhusu hatari, vitisho na mashambulizi ya maharamia wa baharini nchini Somalia.

Yury Fedotovo amegusia hatari zinazosababishwa na mashambulizi ya maharamia wa baharini wa Somalia dhidi ya meli za biashara na kuitaka jamii ya kimataifa ifanye juhudi kubwa zaidi za kupambana na maharamia hao.

Amesema, maeneo mengi ya fukwe za Somalia hayamo katika udhibiti wa maafisa usalama wa serikali ya nchi hiyo kiasi kwamba meli zinazotumia bahari ya Somalia zinalazimika kushauriana kwanza na mashirika ya kimataifa ya safari za baharini badala ya kuwasiliana na maafisa usalama wa Somalia.

Mgogoro wa maharamia ni janga kubwa nchini Somalia

 

Tarehe 13 Machi mwaka huu, maharamia wa Somalia waliishambulia na kuiteka meli ya mafuta ya MT Aris 13 pamoja na mabaharia wake. Hata hivyo mabaharia hao waliachiliwa huru baada ya ufyatulianaji risasi na mazungumzo.

Tarehe 23 Machi mwaka huu, maharamia wa Soamalia waliishambulia meli ya uvuvi ya Asayr 2. Licha ya kuachiliwa huru mabahari wa meli hiyo, lakini maharamia wa Somalia wangali wanaishikilia meli hiyo kwa lengo la kuitumia katika kuzivamia na kuzishambulia meli nyingine.