Watoto nusu milioni waakabiliwa na lishe duni kaskazini mashariki mwa Nigeria
Watoto takribani nusu milioni wanakabiliwa na lishe dunia kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Peter Lundberg naibu mratibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu Nigeria amesema, iwapo misaada haitafika haraka, mtoto moja kati ya watano walio na lishe duni atafariki.
Aidha amesema iwapo zaidi ya Wanigeria milioni moja walioathiriwa na ugaidi wa kundi la Boko Haram watakabiliwa na njaa iwapo misaada ya kimataifa itakatwa katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema ni asilimia 15 tu ya misaada inayohitajika imetolewa na jamii ya kimataifa kuwasiadia watu wa kaskazini mashariki mwa Nigeria wanaokabiliwa na baa kubwa la njaa. Amesema ili kukidhi mahitaji ya miezi sita ijayo, kuna haja ya msaada wa dharura wa dola milioni 242.
Wiki iliyopita Adrian Edwards msemaji wa Kamisheni ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa alitahadharisha kuhusu uwezekano wa watu wengi kupoteza maisha kutokana na njaa Afrika. Alitaja maeneo yanayokabiliwa na njaa kuwa ni pamoja na Pembe ya Afrika, Nigeria na pia Yemen.