Save the Children: Utapiamlo mkali unatia wasiwasi nchini Somalia
Shirika la kimataifa la Save the Children limetangaza kuwa, kiwango cha utapiamlo mkali kinachoshuhudiwa nchini Somalia kinatia wasiwasi.
Ripoti iliyotolewa na shirika la Save the Children imesema kuwa, timu ya shirika hilo imefanya uchunguzi katika maeneo sita ya baadhi ya mikoa iliyokumbwa na mgogoro ya Somalia na kubaini kuwa wastani wa utapiamlo mkali katika baadhi ya maeneo hayo unatia wasiwasi mkubwa.
Ripoti hiyo imesema, majini ya chini ya asilimia 10 ya watoto wanaosumbuliwa na utapiamlo mkali ndiyo yaliyosajili hadi sasa kwa ajili ya misada ya chakula na kwamba iwapo hakutachukuliwa hatua za haraka za kudhamini chakula, watoto hao wa Somalia watanyemelewa na kifo cha kimyakimya.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Save the Children nchini Somalia, Hassan Saadi Nour amesema kuwa, nchi hiyo inakaribia kutumbukia katika maafa makubwa na kwamba vifo vya robo tatu ya wanyama na uhaba wa maji vimezidisha hali mbaya ya Somalia.
Somalia ambayo imekuwa kwenye vita vya ndani kwa zaidi ya miongo miwli kwa sasa inasumbuliwa na ukame mkubwa unaoandamana na njaa.