7 wauawa hotelini katika hujuma ya wabeba silaha huko Kodivaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2986-7_wauawa_hotelini_katika_hujuma_ya_wabeba_silaha_huko_kodivaa
Kwa akali watu 7 wameuawa baada ya kundi la watu waliokuwa na silaha kuvamia hoteli moja ya kifahari mjini Abidjan nchini Ivory Coast.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 13, 2016 16:49 UTC
  • 7 wauawa hotelini katika hujuma ya wabeba silaha huko Kodivaa

Kwa akali watu 7 wameuawa baada ya kundi la watu waliokuwa na silaha kuvamia hoteli moja ya kifahari mjini Abidjan nchini Ivory Coast.

Mashuhuda wanasema kundi hilo la wabeba silaha ambao walikuwa wamefunika nyuso zao wameshambulia kwa risasi hoteli ya kifahari ya L’Etoile du Sud (Southern Star) katika ufukwe wa Grand Bassam mjini Abidjan. Habari zinasema kuwa, hoteli hiyo ya kitalii mara nyingi huwa na wateja raia wa kigeni.

Dramane Kima, mmoja wa mashuhuda hao ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, wavamizi hao walikuwa wanne na kwamba yeye binafsi ameona miili ya watu 7 waliouawa hotelini hapo katika hujuma hiyo ya Jumapili. Hata hivyo takwimu hizo hazijathibitishwa na vyombo husika vya dola.

Upwa wa Grand-Bassam upo umbali wa kilomita 40 mashariki mwa mji wa kibiashara wa Abidjan.

Ni vyema kuashiria hapa kuwa, mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya hoteli za kifahari katika miji mikuu ya Mali na Burkina Faso yalisababisha makumi ya watu kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa.