Trump ataka kufichwa picha za vituo vya Marekani vilivyoharibiwa na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138186-trump_ataka_kufichwa_picha_za_vituo_vya_marekani_vilivyoharibiwa_na_iran
Donald Trump, Rais wa Marekani, amezitaka kampuni za satalaiti kuficha picha za vituo na kambi za kijeshi za Marekani zilizoharibiwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Asia ya Magharibi.
(last modified 2026-05-05T11:51:52+00:00 )
May 05, 2026 11:44 UTC
  • Trump ataka kufichwa picha za vituo vya Marekani vilivyoharibiwa na Iran

Donald Trump, Rais wa Marekani, amezitaka kampuni za satalaiti kuficha picha za vituo na kambi za kijeshi za Marekani zilizoharibiwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Asia ya Magharibi.

Ana Kasparian, mwandishi wa habari wa Marekani, amesema katika kipindi cha televisheni kwamba serikali ya Trump imeyaomba makampuni binafsi ya satalaiti kuficha picha za vituo vya Marekani vilivyoharibiwa katika mashambulizi ya Iran Asia Magharibi.

Katika muktadha huo, kampuni ya upigaji picha za satalaiti ya Planet Labs ilitangaza mwezi uliopita kwamba, kwa ombi la serikali ya Donald Trump, itasitisha uchapishaji wa picha za satalaiti kutoka maeneo yanayohusika katika vita na Iran hadi mwisho wa vita.

Wakati huohuo, Ted Lieu, mwakilishi wa chama cha Democratic katika Bunge la Marekani, amekiri kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliweza kutoa vipigo vikubwa dhidi ya kambi na vituo vya Marekani katika eneo la Asia ya Magharibi.