Uganda yakosolewa kutuma wafanyakazi 1,000 wa afya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30584-uganda_yakosolewa_kutuma_wafanyakazi_1_000_wa_afya_libya
Uganda imetangaza mpango wa kutuma wafanyakazi 1,000 wa sekta ya afya kuhudumu Libya, mpango ambao umekosolewa vikali na wanaharakati wa sekta ya afya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 17, 2017 02:47 UTC
  • Uganda yakosolewa kutuma wafanyakazi 1,000 wa afya Libya

Uganda imetangaza mpango wa kutuma wafanyakazi 1,000 wa sekta ya afya kuhudumu Libya, mpango ambao umekosolewa vikali na wanaharakati wa sekta ya afya.

Milton Turyasiima, kamishna wa huduma za ajira katika wizara ya leba nchini Uganda amesema mji wa Benghazi ambao ni wa pili kwa ukubwa Libya umeiomba Uganda iwatume wafanyakazi wa sekta ya afya katika mji huo. Amesema serikali inachunguza ombi hilo hasa usalama wa wafanyakazi na mazingira ya kikazi.

Hata hivyo wanaharakati wa sekta ya afya wamekosoa mpango huo wakisema Uganda yenyewe ina uhaba wa wahudumu wa afya.

Asia Russel mwanaharakati wa Afya amesema kuna uhaba mkubwa wa wafanyakazi wa sekta ya afya jambo ambalo hupelekea watu wengi wa Uganda kupoteza maisha kila siku hivyo mpango huo wa serikali haufai hata kidogo.

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, nchi nyingi za Mashariki ya Kati zimekuwa zikiwaajiri raia wa Afrika Mashariki hasa Kenya na Uganda na kuwalipa mishahara duni.