Jun 18, 2017 03:52 UTC
  • Jeshi la Mali lashambuliwa, askari watano wauawa

Wanajeshi watano wa Mali wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa katika shambulio lilofanywa na watu wenye silaha jana Jumamosi katika kambi moja ya jeshi la Mali kaskazini mwa nchi hiyo.

Jeshi la Mali limeashirika katika ripoti yake kwamba wanajeshi waliojeruhiwa wamepelekwa katika mji wa Timbuktu na kuongeza kuwa wahusika wa shambulizi hilo hawajatambuliwa hadi sasa. Jeshi la Mali limetangaza pia kwamba magari yao saba yameharibiwa kwenye shambulio la jana. Nacho kikosi cha Umoja wa mataifa kilichopo Mali kimeandika katika ukurasa wake wa Twitter bila ya kutoa maelezo kuhusu shambulio hilo kwamba: jeshi la Mali limekumbwa na shambulio la umwagaji damu.

Kikosi cha kudumisha amani cha UN nchini Mali 

Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo, hata hivyo kundi la kigaidi la Boko Haram lina rekodi ya muda mrefu ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya jeshi la Mali na raia wa nchi hiyo. 

Tags