Tahadhari kuhusu hali ya watoto mashariki mwa Ethiopia
Shirika la madaktari wasio na mipaka wameonya kuhusu hali mbaya ya watoto wadogo mashariki mwa Ethiopia.
Mtandao wa Intaneti wa Le Monde wa nchini Ufaransa umeripoti taarifa ya shirika hilo la madaktari wasio na mipaka (MSF) na sambamba na kuonya kuhusu hali mbaya ya watoto wadogo katika eneo la Pembe ya Afrika linalojumuisha Somalia na mashariki mwa Ethiopia na kuongeza kuwa, idadi ya watoto wadogo wanaosumbuliwa na lishe duni katika eneo hili mwaka huu wameongezeka mara kumi ikilinganishwa na wakati huo mwaka 2016.
Shirika la MSF limeongeza kuwa, khumusi ya watoto 67 waliolazwa katika hospitali mbalimbali nchini Ethiopia wamepoteza maisha yao kutokana na lishe duni katika wiki mbili za awali za mwezi Juni.
Shirika hilo limeongeza kuwa, karibu watu milioni saba na laki nane wa jamii ya watu milioni moja ya Ethiopia wanahitajia misaada ya haraka ya chakula.
Jamii ya kimataifa hivi sasa imetenga dola milioni 302 na serikali ya Ethiopia imetenga dola milioni 766 kwa ajili ya kupambana na mgogoro wa njaa nchini humo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, bado kunahitajika dola milioni 481 nyingine kwa ajili ya kupambana na mgogoro wa njaa nchini Ethiopia.