Wapinzani Sudan Kusini wameituhumu serikali kuushambulia mji wa Aburok
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34321-wapinzani_sudan_kusini_wameituhumu_serikali_kuushambulia_mji_wa_aburok
Wapinzani nchini Sudan Kusini wamevituhumu vikosi vya serikali kuwa vimeushambulia mji unaowahifadhi maelfu ya wakimbizi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 13, 2017 23:24 UTC
  • Wapinzani Sudan Kusini wameituhumu serikali kuushambulia mji wa Aburok

Wapinzani nchini Sudan Kusini wamevituhumu vikosi vya serikali kuwa vimeushambulia mji unaowahifadhi maelfu ya wakimbizi.

Lam Paul Gabriel msemaji wa wapinzani wa Sudan Kusini amesema kuwa shambulio lililofanywa na jeshi la nchi hiyo katika mji wa Aburok kaskazini mwa nchi ni hatua ya kigaidi. 

Lam Paul Gabriel, Msemaji wa wapinzani wa Sudan Kusini  

Mji wa Aburok ni moja ya makao yaliyosalia ya wanamgambo wenye misimamo mikali huko kaskazini mwa Sudan Kusini. Mji wa Aburok ambao unapatikana karibu na mpaka na Sudan unawahifadhi karibu watu elfu kumi ambao wamelazimika kuwa wakimbizi mara kadhaa kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan Kusini. Hii ni katika hali ambayo serikali ya Juba imetangaza kuwa vikosi vyake havifanyi shambulizi iwapo lengo lao si kujilinda. Kundi la madaktari wasio na mipaka lililoko Sudan Kusini limetahadharisha kuwa wakazi wa mji wa Aburok wanakabiliwa na hatari kubwa.