Jan 03, 2018 07:48 UTC
  • Mateka 700 waachiwa huru kutoka mikononi mwa Boko Haram

Maafisa wa jeshi la Nigeria wametangaza kuwa watu 700 waliokuwa wametakwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo wameachiwa huru.

Kanali Timoth Antiga msemaji wa divisheni ya 8 ya jeshi la Nigeria amesema kuwa mateka hao walioachiwa huru ni pamoja na wakulima, wavuvi na watu kutoka familia mbalimbali ambao walikuwa wakitumiwa vibaya kama watumwa na kundi la Boko Haram. Msemaji huyo wa jeshi la Nigeria ameongeza kuwa raia hao wameachiwa huru kufuatia oparesheni iliyofanywa dhidi ya Boko Haram katika eneo la Ziwa Chad. 

Wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram 

Kanali Antiga ameongeza kueleza kuwa jeshi la Nigeria linawahoji raia hao walioachiwa huru ili kupata taarifa zaidi kuhusu maficho na kambi za kundi hilo la kigaidi. Kundi la kigaidi la Boko Haram lilianza kubeba silaha mwaka 2009 kwa lengo la kile ilichokitaja kuwa ili kuasisi dola la Kiislamu huko kaskazini mwa Nigeria na kisha kuendeleza mashambulizi yake huko Niger, Chad na kaskazini mwa Cameroon. Watu zaidi ya elfu 20 wameuawa na kundi hilo la kigaidi huko Nigeria, Cameroon na Chad na wengine zaidi ya milioni mbili wamelazimika kuyahama makazi yao kufuatia kushtadi mashambulizi na hujuma za kundi hilo. 

Tags