Wahajiri 25 waaga dunia katika ajali ya boti pwani ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i38627-wahajiri_25_waaga_dunia_katika_ajali_ya_boti_pwani_ya_libya
Kwa akali wahajiri 25 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama wakiwa katika safari ya kwenda Ulaya, katika bahari ya Mediterania, katika pwani ya Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 07, 2018 04:20 UTC
  • Wahajiri 25 waaga dunia katika ajali ya boti pwani ya Libya

Kwa akali wahajiri 25 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama wakiwa katika safari ya kwenda Ulaya, katika bahari ya Mediterania, katika pwani ya Libya.

Timu mbili za uoakoaji zimesema boti hiyo ya pastiki ilikuwa imebeba wahajiri wapata 150 kabla ya kuzama mashariki mwa mji mkuu Tripoli.

Kadhalika askari wa Gadi ya Pwani ya Italia wametangaza habari ya kuwaokoa wahajiri 85 katika ajali hiyo ya jana Jumamosi.

Shirika la Spanish Charity Proactiva Open Arms limesema wapiga mbizi wake wanaendelea na operesheni ya kusaka miili zaidi, lakini wameeleza wasi wasi wao kuwa yumkini watapata maiti chache ikilinganishwa na idadi kamili ya wahajiri waliozama.

Wahajiri wa Kiafrika wakiwa safarini kuelekea Ulaya

Kwa mujibu wa Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, zaidi ya wakimbizi elfu tatu waliaga dunia mwaka jana wakijaribu kufika Ulaya kupitia Bahari ya Mediterania, vifo ambavyo vingi vilitokea katika njia ya bahari kutoka Libya kuelekea Italia. 

Mwaka juzi 2016 zaidi ya wahajiri elfu tano aghalabu yao wakiwa wa Kiafrika walipoteza maisha katika safari hizo hatari.