SAUTI, Waislamu watakiwa kuyaenzi mafundisho ya Qur'an Tukufu na kuacha mifarakano
Waislamu duniani wametakiwa kuenzi mafundisho ya Qur'an Tukufu sambamba na kuachana na tofauti ndogondogo zinazoweza kuwafanya kutokuwa wamoja.
Hayo yamesemwa na washiriki wa kongamano la Kiislamu lililofanyika mjini Kampala, Uganda ambapo pamoja na mambo mengine wametakiwa kufungamana na wito wa Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu hicho.
Katika hatua nyingine washiriki wa kongamano hilo wamelaani vikali tangazo la hivi karibuni la Rais Donald Trump wa Marekani la kuutaja mji wa Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni na wameutaka Umoja wa Mataifa kuzuia harakati hizo za Kizayuni huko Palestina.
Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Kampala, Kigozi Ismail kwa taarifa kamili............../