Yumkini Uganda ikarejesha adhabu ya kifo (SAUTI)
Jan 19, 2018 13:06 UTC
Kuna wafungwa 278 ambao wamehukumiwa kifo lakini Rais Museveni hajatia saini amri ya utekelezwaji wa hukumu hizo.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema anatafakari kurejesha hukumu ya kifo nchini humo ili kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu nchini. Rais Museveni amesema amekuwa akisita kutia saini kila hukumu ya kifo anayoletewa tokea mwaka 1999. Hatua hiyo imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa Waganda, baadhi wakiunga mkono kurejeshwa kwa adhabu hiyo huku wengine wakipinga.
Mwandishi wetu wa Kampala, KIGOZI ISMAIL ana maelezo zaidi.........
Tags