Feb 03, 2018 07:48 UTC
  • Makamanda 23 wanaomuunga mkono Anan watiwa mbaroni Misri

Idaya ya usalama nchini Misri imewatia mbaroni makamanda 23 miongoni mwa wafuasi wa Sami Hafez Anan, mkuu wa zamani wa majeshi nchini humo ambaye alitangaza azma yake ya kutaka kugombea uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa habari za ndani, makamanda hao walitiwa mbaroni siku ambayo Anan alitiwa mbaroni na faili lake la kughushi nyaraka na uchochezi wa askari, kukabidhiwa kwa mwendesha mashtaka wa Misri. Inaelezwa kwamba, tuhuma inayowakabili makamanda hao ni kumuunga mkono mkuu huyo wa zamani wa majeshi. Kabla ya hapo yapata siku 10 zilizopita kamanda mkuu wa sasa wa majeshi ya Misri sambamba na kutoa taarifa ya ukosoaji dhidi ya Sami Hafez Anan ya kutaka kugombea katika uchaguzi ujao, aliitaja kuwa inayokinzana na sheria.

El-Sisi, fotokopi ya Hosni Mubarak nchini Misri

Aliongeza kuwa, bila ya kupata ridhaa kutoka kwa jeshi la taifa au kutekeleza hatua za lazima alikurupuka na kutangaza azma yake ya kugombea urais, na kwamba hata katika matamshi yake ya kutangaza nia yake hiyo aliwachochea askari wa Misri wafanye uasi. Uchaguzi wa rais nchini Misri umepangwa kufanyika tarehe 26-27 na 28 za mwezi Machi mwaka huu. Watakaochuana katika uchaguzi huo ni Rais Abdel Fattah el-Sisi anayetetea kiti chake na Musa Mustafa Musa wa chama cha Ghad ambaye anatajwa kuwa aliyechaguliwa na el-Sisi mwenyewe kuchuana naye.

Tags