Mar 06, 2018 08:07 UTC
  • UNICEF: Nchi za Afrika zinaongoza kwa ndoa za utotoni

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa Unicef umesema ingawaje tabia ya kuozwa kwa lazima mabinti wadogo imepungua duniani, lakini nchi za chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika kwa sasa zinaongoza kwa uozo huo.

Anju Malhotra, Mshauri wa masuala ya Jinsia wa Unicef amesema moja kati ya ndoa tatu za watoto wadodo duniani inafanyika katika nchi za chini ya Jangwa la Sahara, uozo wa jamii ambao ulikuwa umeshika kasi katika nchi za kusini mwa bara Asia.

Hata hivyo amesisitiza kuwa, takwimu hizo zinaashiria upungufu wa ndoa hizo, ikilinganishwa na muongo mmoja uliopita, ambapo ilikuwa ndoa moja kati ya tano za watoto wadogo duniani.

Wanafunzi wa Chibok waliokuwa wametekwa nyara na Boko Haram, baadhi yao waliolewa kwa nguvu

Amesema kuna haja ya elimu kutumiwa kupiga vita ndoa hizo za utotoni katika nchi hizo za Afrika, huku akiwataka viongozi wa dunia kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi waliyotoa, ya kutokomeza ndoa hizo duniani kufikia mwaka 2030, chini ya mwavuli wa Malengo ya Maendeleo-Endelevu ya Umoja wa Mataifa SDG's .

Ripoti ya Unicef inasema kuwa, binti mmoja kati ya watano kote duniani analazimishwa kuingia kwenye ndoa kabla ya kutimiza miaka 18.

Tags