Wanafunzi 38 wapoteza maisha katika ajali ya basi Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i41597-wanafunzi_38_wapoteza_maisha_katika_ajali_ya_basi_ethiopia
Watu 38 wamepoteza maisha nchini Ethiopia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika mtaro mkubwa katika jimbo la Amhara kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 13, 2018 12:15 UTC
  • Wanafunzi 38 wapoteza maisha katika ajali ya basi Ethiopia

Watu 38 wamepoteza maisha nchini Ethiopia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika mtaro mkubwa katika jimbo la Amhara kaskazini mwa nchi hiyo.

Shirika la Utangazaji la Fana limeripoti leo Jumanne kuwa basi hilo liliondoka katika mkondo wake na kutumbukia katika mtaro na kuua watu 38. Watu wengine 10 wamejeruhiwa.  

Taarifa zinasema aghalabu ya waliopoteza maisha au kujeruhiwa ni wanafunzi wa chuo kikuu. Ajali hiyo imetokea katika wilaya ya Debub Wollo katika jimbo la Amhara.

Ethiopia hivi sasa iko mbioni kukarabati barabara zake zilizochakaa lakini wataalamu wanasema uendeshaji mbaya wa magari pamoja na hali mbaya ya kiufundi ya magari mengi ndio chanzo kikuu cha vifo katika barabara za nchi hiyo.

Ripoti inasema, watu zaidi ya 16,000 walipoteza maisha katika ajali za barabarani nchini Ethiopia kati ya mwaka 2014 na 2017.