Rais wa Zimbabwe awasamehe wafungwa 3,000
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i42022-rais_wa_zimbabwe_awasamehe_wafungwa_3_000
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye alichukua madaraka baada ya mtangulizi wake Robert Mugabe kulazimishwa kujiuzulu mwezi Novemba mwaka jana, amewasamehe wafungwa zaidi ya 3,000 kwa lengo la kupunguza msongamano mkubwa kwenye magereza ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 22, 2018 11:06 UTC
  • Rais wa Zimbabwe awasamehe wafungwa 3,000

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye alichukua madaraka baada ya mtangulizi wake Robert Mugabe kulazimishwa kujiuzulu mwezi Novemba mwaka jana, amewasamehe wafungwa zaidi ya 3,000 kwa lengo la kupunguza msongamano mkubwa kwenye magereza ya nchi hiyo.

Msamaha huu wa rais wa Zimbabwe utashuhudia kuachiwa kwa wafungwa wote wa kike walemavu huku waliohukumiwa kifungo cha maisha jela wakiwa hawahusiki na msamaha huo. Wafungwa wanaoumwa na wale ambao wamezidi umri wa miaka 60 na ambao wametumikia robo tatu ya kifungo chao pia wataachiwa huru. “Rais kwa kufuata katiba ya Zimbabwe ametoa msamaha kwa wafungwa,” imesema taarifa ya idara ya magereza nchini humo.Taarifa hiyo ya Jumatano imesema kuwa jumla ya wafungwa 3,000 wataachiwa huru na kufanya idadi ya wafungwa waliobakia kufikia elfu 17.

Wafungwa Zimbabwe

Serikali ya Zimbabwe inakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha unaoifanya ishindwe kuwahudumia kwa chakula na nguo pamoja na matibabu maelfu ya wafungwa ambapo mwaka 2013 jumla ya wafungwa 100 walipoteza maisha wakiwa gerezani.