Wafanyakazi 10 wa UN watoweka Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43696-wafanyakazi_10_wa_un_watoweka_sudan_kusini
Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa wafanyakazi wasiopungua 10 wa umoja huo nchini Sudan Kusini wametoweka na hawajulikani waliko.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 26, 2018 23:30 UTC
  • Wafanyakazi 10 wa UN watoweka Sudan Kusini

Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa wafanyakazi wasiopungua 10 wa umoja huo nchini Sudan Kusini wametoweka na hawajulikani waliko.

Ellen Noodieau anayesimamia operesheni za misaada ya kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesema kuwa, wafanyakazi 10 wa umoja huo walitoweka jana katika maeneo ya kusini magharibi mwa Sudan Kusini na kwamba kuna uwezekano mkubwa wametekwa nyara. 

Noodieau ameeleza wasiwasi wake kuhusu tukio hilo na kusema: Kuna udharura wa kupatikana habari kuhusu hali ya wafanyakazi hao wa UN nchini Sudan Kusini haraka iwezekanavyo. 

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakishambuliwa au kutekwa nyara nchini Sudan katika kipindi chote cha miaka minne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. 

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inasema hii ni mara ya pili kwa wafanyakazi wa umoja huo kutekwa nyara na makundi ya waasi nchini Sudan Kusini katika mwezi huu wa Aprili.